Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma Waaswa Kuongeza Ufanisi


Watendaji Wakuu wa taasisi za umma wameaswa kuongeza ufanisi wa taasisi wanazoziongoza na hivyo kupunguza utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali Kuu.

 

Maelekezo hayo yaliyotolewa Jumatatu, Julai 28, 2025, na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka wakati akifungua mafunzo elekezi kwa wakuu wa taasisi za umma 114 yaliyofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha Pwani. Aidha, Balozi Dkt. Kusiluka aliwasisitiza viongozi hao kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kudhibiti matumizi yasiyo na tija ya fedha za umma pamoja na kujenga uwezo wa taasisi wanazosimamia kwenye maeneo ya rasilimali watu, teknolojia na miundombinu.

 

Vilevile, alizitaka taasisi za umma kila moja kwa nafasi yake kuhakikisha zinashiriki kikamilifu katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.