Habari
KATIBU MKUU KIONGOZI AWAALIKA WANANCHI KUTEMBELEA MAONESHO YA NANE NANE 2024, NZUGUNI - DODOMA
KATIBU MKUU KIONGOZI AWAALIKA WANANCHI KUTEMBELEA MAONESHO YA NANE NANE 2024, NZUGUNI - DODOMA
Katibu Mkuu Kiongozi Mheshimiwa Balozi Dkt. Moses Kusiluka ameipongeza Wizara ya Kilimo pamoja na Taasisi zake kwa maandalizi mazuri ya Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane alipotembelea na kujionea Teknolojia mpya za uzalishaji pamoja na Tafiti mbali mbali za Kilimo.
Mh. Balozi Dkt. Kusiluka ameyasema hayo leo tarehe 6 Agosti, 2024 alipotembelea katika Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma, akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe.
Aidha Katibu Mkuu Kiongozi amewaalika wananchi kuja katika Maonesho hayo kujifunza Teknolojia mbali mbali za kilimo na ufugaji pamoja na mnyororo mzima wa thamani.
Kwa upande mwingine Mh. Balozi Dkt. Kusiluka amesema kuwa hivi sasa kilimo ni biashara kubwa na teknolojia zinazotumika ni za kisasa ambapo ametoa wito kwa vijana kujishughulisha na kilimo hususan katika usindikaji wa kisasa wa bidhaa za kilimo kwa kuwa kina fursa kubwa za kiuchumi.