Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

Balozi Hussein Athman Kattanga Aapishwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 1 April, 2021 amemuapisha Balozi Hussein Athman Kattanga na kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

 Hafla ya kumuapishwa Balozi Hussein Athman Kattanga, imefanyika Ikulu ya Chamwino, wilayani Chamwino, mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Philip I. Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Spika Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mawaziri, Makatibu Wakuu na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Akizungumza baada ya kuapishwa kwake, Mhe. Balozi Hussein A. Kattanga amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa imani kubwa aliyoionesha kwake kwa kumteua katika wadhifa huo, na ameahidi kutekeleza majukumu yake kwa juhudi na maarifa, kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa.

“Mheshimiwa Rais, Kazi za Katibu Mkuu Kiongozi ni kuratibu shughuli za Serikali katika Wizara na Taasisi zake zilizowekwa ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa kazi. Ili kufikia dira yam waka 2025 ni lazima Wizara na Taasisi za serikali zifanye kazi kwa pamoja ili kufikia malengo tuliyojiwekea”, aliseongeza Mhe. Balozi  Kattanga.