Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Kabla ya Uteuzi huo, Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India. Uteuzi huu unaanza Mara moja. Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine.