Habari
Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amteua Dkt. Moses Mpogole Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Kiongozi - 03/01/2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 03/01/2023 amemteua Dkt. Moses Mpongole Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Dkt. Kusiluka anachukua nafasi iliyoachwa na mtangulizi wake Balozi Hussein Athuman Kattanga ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York, nchini Marekani na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Kusiluka alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Ikulu.