Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

Makatibu wakuu, manaibu waapishwa


Rais Jakaya Kikwete amewaapisha makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu wapya wa wizara mbalimbali aliowateua juzi, ambapo wengi wameahidi kushiriki kikamilifu katika kufanikisha kwa kusimamia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Makatibu hao waliapishwa jana kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam, ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo baadhi ya mawaziri wa wizara zao pamoja na wageni waalikwa walishuhudia tukio hilo.

Makatibu wakuu walioapishwa ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Jumanne Sagini, Dk Servacius Likwelile Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dk Patrick Makungu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi. Dk Shaaban Mwinjaka, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Uledi Mussa.

Wengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Kidata, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Charles Pallangyo, Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Anna Maembe.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni, Sihaba Nkinga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Sophia Kaduma.

Naibu Makatibu wakuu wapya wizara zao katika mabano ni Angelina Madete (Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira), Regina Kikuli (Ofisi ya Waziri Mkuu), Profesa Adolf Mkenda (Wizara ya Fedha-Sera), Dorothy Mwanyika (Wizara ya Fedha-Fedha za Nje na Madeni), Rose Shelukindo (Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa).

Wengine ni Zuberi Samataba (Ofisi ya Waziri Mkuu-Tamisemi anayeshughulika na Elimu), Edwin Kiliba (Ofisi ya Waziri Mkuu-Tamisemi), Dk Yamungu Kayandabila (Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika), Dk Selassie Mayunga (Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Monica Mwamunyange (Wizara ya Uchukuzi).

Consolata Mgimba (Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Dk Deodatus Mtasiwa ( Tamisemi afya),Profesa Elisante ole Laizer (Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo) na Armantius Msole (Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki).

Profesa Sifuni Mchome ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), hakuwepo katika kiapo,haikuelezwa bayana sababu ya kukosekana kwake katika hafla hiyo.

PRESIDENT Jakaya Kikw ete swears-in the new Permanent Secretary in the Ministry for Information, Youth, Culture and Sports, Ms Sihaba Nkinga at the State House in Dar es Salaam on Friday. Looking on (second left) is Chief Secretary Ambassador Ombeni Sefue. (Photo by Staff)

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akimuapisha Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Habari ,Vijana , Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga (kulia) leo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makatibu wakuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.