Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

MKUTANO WA 12 WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA AMBAZO NI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA WAFUNGWA, 15 JULAI, 2015


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo tarehe 15 Julai, 2015 ameelezea furaha yake kutokana na mafanilio makubwa ya Mkutano wa 12 wa Wakuu wa Nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola ulioanza juzi tarehe 13 Julai, 2015. Tumekuwa na Mkutano mzuri na wa mafanikio, alisema. Tumejadiliana, tukaainisha msuala muhimu yahusuyo utekelezaji wa Sera na mikakati na kukubaliana juu ya hatua za kuchukua kukabiliana na changamoto mbalimbali. Balozi Sefue aliyasema hayo wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufunga mkutano huo.

Akifunga Mkutano huo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini, aliishukuru Jumuiya ya Madola pamoja na Wakuu wa Utumishi wa Umma kwa heshima kubwa waliyoipatia Tanzania kuandaa mkutano huo muhimu.

Ninaamini mmekuwa na mkutano mzuri na kwamba mtakwenda kutekeleza hatua mbalimbali mlizoazimia katika kuboresha utekelezaji wa Sera na mikakati ya kuwatelea maendeleo wananchi, alisema.

 

NB: Hotuba kamili ya Mhe. Dkt. Mwadini inapatikana katika tovuti hii