Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI OMBENI Y. SEFUE, ATEMBELEWA NA NAIBU BALOZI WA MAREKANI NCHINI, BI VIRGINIA M. BLASER - 25 JUNI, 2015.


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue leo tarehe 25 Juni, 2015 ametembelewa na Naibu Balozi wa Marekani nchini, Bi Virginia M. Blazer ofisini kwake Ikulu, Dar es Salaam na kuwa na mazungumzo ya ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani hasa kuhusiana na programu ya Ikulu ya Marekani (State House Fellows Program) katika kuwajengea uwezo vijana wa Tanzania katika masuala ya vipaumbele vya maendeleo ya Taifa hasa katika Kilimo na kuwawezesha katika mbinu za uongozi.

Programu hiyo ni endelevu na itakuwa ikifanyika kila mwaka kwa vijana wa Tanzania na Marekani kujengeana uwezo wa kiuongozi na masuala ya kimaendeleo kwa ujumla.

Balozi Sefue alielezea kufurahishwa kwake na kuishukuru Serikali ya Marekani kwa msaada unaotolewa kupitia programu hiyo, ambayo kwa kuanzia imetoa ufadhili wa nafasi za masomo kwa vijana kumi (10) wa Tanzania katika masuala ya kilimo na uongozi.