Habari
KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI Y. SEFUE ATEMBELEWA NA MKURUGENZI WA KANDA WA HAVARD BUSINESS REVIEW, BI. MAXINE GORDON, 31 JULAI, 2015.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue leo tarehe 31 Julai, 2015 alitembelewa na Mkurugenzi wa Kanda wa “Havard Business Review (HBR)” ambayo ni kampuni ya machapisho ikiwa na makao makuu mjiniNew York, Marekani. Machapisho ya “HBR” yanaheshimikasana na kusomwa duniani kote.
Bi. Gordon aliambatana na Bw. Omar El Asfari na Bi. Diana Lopez, wote kutoka wakala ya kampuni hiyo na ambao kwa pamoja wapo nchini kwa ajili ya kuchapisha taarifa maalumu (Special Edition) kuhusu mafanikio ya Awamu ya Nne ya Uongozi chini ya Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Wawakilishi hao wamekwishafanya mahojiano na Mheshimiwa Rais kabla ya safari yake ya kikazi nchiniAustraliana wanaendelea kuwahoji Watendaji mbalimbali waandamizi ndani ya Serikali na Taasisi zake, ikiwa ni pamoja na wakuu wa taasisi binafsi.
Katibu Mkuu Kiongozi amekubali ombi la kuwa na mahojiano na wawakilishi hao kwa tarehe itakayopangwa baadaye.