Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI Y. SEFUE ASHUHUDIA UZINDUZI WA "EAC VIDEO CONFERENCE FACILITY" 20 FEBRUARI, 2015


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo tarehe 20 Februari, 2015 amejumuika na viongozi na watumishi wa Wizara ya Afrika Mashariki katika kushuhudia uzinduzi Mfumo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Uendeshaji wa Mikutano kwa njia ya Mtandao (EAC Video Conference Facility).

Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo ambapo Katibu Mkuu Kiongozi alipata fursa ya kuwasiliana moja kwa moja na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, akiwa anazindua mfumo huo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta, mjini Nairobi.

Baada ya uzinduzi huo, Katibu Mkuu Kiongozi alielezea kufurahishwa kwake na teknolojia ya uendeshaji wa mikutano kwa njia ya mtandao ambapo alisema inawezesha sio tu ufanisi katika utendaji kazi, bali pia inasaidia kupunguza gharama na muda wa kuhudhuria mikutano, inasaidia kuweka kumbukumbu sahihi za mikutano na kuongeza tija katika utendaji kazi.