Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI OMBENI Y. SEFUE ASHIRIKI KATIKA HAFLA YA MHESHIMIWA RAIS, DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE YA KUWEKA SAINI KWENYE MISWADA YA SHERIA, DAR ES SALAAM, 04 AGOSTI, 2015


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo tarehe 4 Agosti, 2015 amejumuika na Viongozi mbalimbali Waandamizi na watumishi wa umma katika Hafla ya Mheshimiwa Rais ya uwekaji saini kwenye miswada mitano ya sheria iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano mwezi Julai 2015. Hafla hiyo ya aina yake ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ikulu.

 

Miswada mitano iliyowekwa saini na Mheshimiwa Rais ni (i) Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 (ii) Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi ya Mwaka 2015  (iii) Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi ya Mwaka 2015 (iv) Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu ya Mwaka 2015 na (v) Sheria ya Masoko ya Bidhaa ya Mwaka 2015.

 

Balozi Sefue alimkaribisha Mheshimiwa Rais kutekeleza jukumuhilola kihistoria na kumwelezea Mheshimiwa Rais kuwa ametimiza vema ahadi zake kwa wananchi kwa kuwa amejibu kilio cha muda mrefu cha walimu cha kuwa na Tumeyaona pia amejibu kilio cha muda cha wakulima cha kuwa na masoko ya bidhaa. Aidha, Balozi Sefue alimwelezea Rais kuwa ameweka misingi imara kwenye sekta madini, mafuta na gesi, misingi ambayo ni ya uwazi na uwajibikaji utakaosaidiaTanzaniakufikia uchumi wa kati kwa miaka michache ijayo.

 

Katibu Mkuu Kiongozi ametoa rai kuwa njia bora ya kuenzi kazi nzuri iliyofanywa na Rais Kikwete itakuwa ni kuendeleza kwa ufanisi mkubwa misingi yote imara aliyoiwekeza na kuisimamia kwa dhati.