Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI OMBENI Y. SEFUE AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI, MHE. DIANNA MELROSE 13 JANUARI, 2015


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo tarehe 13 Januari, 2015 amefanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza, Mhe. Dianna MELROSE.

Katika Mazungumzo hayo, Mhe. Melrose aliambatana na Bw. Vel GNANENDRAN, Mkuu wa Ofisi ya Ushirikiano wa Kimaendeleo ya Serikali ya Uingereza hapa nchini (DFID), ambaye alitumia fursa hiyo kujitambulisha rasmi kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Mazungumzo yao yaligusia masuala yanayohusu uwekezaji wa kampuni za Uingereza katika sekta ya gesi asilia na chamgamoto zilizopo, kubwa ikiwa ni mchakato wa kupata ardhi kwa ajili ya mitambo ya uchakataji na usindikaji wa gesi asilia (LNG), maandalizi ya Uchaguzi Mkuu na Kura ya Maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa na mwisho ni ufafanuzi kuhusu muamala wa “ESCROW”.

Katibu Mkuu Kiongozi alitoa ufafanuzi ambao ujumbe huo ulihitaji na kuahidi kufuatilia kila ahadi iliyotolewa na Serikali katika kushughulikia masuala hayo.

Aidha, mara baada ya kumaliza mkutano huo, Balozi Sefue alikutana na ujumbe mwingine kutoka Kampuni ya “Oryx Energies” ulioongozwa na Bw. Vaughan GIBSON kutoka Oryx Energies, Geneva, ambao nao walizungumzia masuala ya uwekezaji katika nishati wakiwa ni wabia katika Kampuni ya “TIPER”.