Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI OMBENI Y. SEFUE, AHUDHURIA HAFLA YA KUMKARIBISHA RASMI MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI, PROFESA MUSSA J. ASSAD, ILIYOFANYIKA MOROGORO KATIKA HOTELI YA NASHERA, JANUARI 8, 2015


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kumkaribisha rasmi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Mussa J. Assad, iliyofanyika mjini Morogoro katika hoteli ya Nashera, Januari 8, 2015.

 

Katika hotuba yake, Balozi Sefue alimpongeza Profesa Assad kwa kuteuliwa kwake kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na akaeleza kuwa Mheshimiwa Rais ana imani kubwasanakwake kuwa ataimudu kazi hiyo. Aidha, aliipongeza Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa utendaji kazi mzuri ambao umeileteaTanzaniasifa kubwa ndani na nje ya nchi.

 

Katibu Mkuu Kiongozi, aliwahimiza watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, kumpa ushirikiano mkubwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili aweze kufanikisha majukumu yake. “ Ni jambo lililo wazi kuwa peke yake Profesa Assad hawezi kufanikiwa; atafanikiwa kwa kadri ya msaada na ushirikiano mtakaompa. Nakuombeni mtoe msaada na ushirikiano huo”, alisisitiza.

 

Katika hafla hiyo, kulifanyika uzinduzi wa mawasiliano ya moja kwa moja ya barua pepe, kati ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, hatua ambayo ilimfurahishasanaKatibu Mkuu Kiongozi.

 

Mwishoni mwa hafla hiyo, watumishi walimkabidhi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na nakala za Miongozo na Sheria zinazohusu masuala ya udhibiti na ukaguzi wa hesabu za serikali.

 

NB: Hotuba nzima ya Katibu Mkuu Kiongozi ipo katika sehemu ya hotuba ya tovuti hii