Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI AZUNGUMZA NA WASHIRIKA WA MAENDELEO (DPS). 8 JANUARI, 2015


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue leo tarehe 8 Januari 2015 amefanya mazungumzo na Washirika wa Maendeleo ikiwa ni sehemu ya utaratibu aliojiwekea wa kukutana na kufafanua masuala mbalimbali yanayoihusu Serikali.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wapatao 15 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Washirika wa Maendeleo, Balozi wa Finland Mhe. Sinikka Antila

Balozi Sefue alitumia fursa hiyo kufafanua kwa kina juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya Sakata la muamala wa Escrow, ambapo maelezo yake yalikidhi kiu ya Washirika wa Maendeleo.

Kwa Ujumla, Washirika wa Maendeleo wameridhishwa na hatua zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa lakini wakaom a Serikali iendelee mara kwa mara kuwapatia taarifa hizi muhimu badala ya kuacha tetesi na uvumi kushamiri.