Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI AWAKARIBISHA WAKUU WA UTUMISHI WA UMMA WA NCHI ZA AFRIKA AMBAZO NI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA, 13 JULAI, 2015


Tarehe 13 Julai, 2015 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue amewakaribisha Wakuu wa Nchi 13 za Afrika ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola wanaohudhuria Mkutano wa 12 wa Wakuu wa Utumishi wa Umma unaofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 13-15 Julai, 2015.

Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa Mkutano huo ambao umefunguliwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano kama huu, ambapo mara ya kwanza ulifanyika Arusha mwaka 2005.

Balozi Sefue aliishukuru Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Utumishi wa Umma kwa heshima hii kubwa waliyoipatia Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano na akaeleza matarajio yake kuwa majadiliano yao ya siku mbili yatasaidia katika kuboresha na kuimarisha Utumishi wa Umma utakaowaletea maisha na huduma bora wananchi.

Mkutano huu unajadili mada kuu: From Good Plans to Effective Execution: Anchoring Policy Coherence, Strategy and Execution for a High Performance Culture in the Public Service, ilisisitizwa kuwa, haitoshi tu kuwa na mipango na mikakati mizuri, umuhimu upo katika kuhakikisha mipango na mikakati hiyo inatekelezwa kikamilifu na kuwaletea maendeleo walengwa kama ilivyokusudiwa.

 

NB: Hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi inapatikana katika tovuti hii