Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI AWAKARIBISHA CHAKULA CHA JIONI, WAGENI KUTOKA MATAIFA YANAYOIBUKIA KATIKA SEKTA YA GESI ASILIA NA MAFUTA DUNIANI. 29 JUNI, 2015.


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue leo tarehe 29 Juni, 2015 amewakaribisha  chakula cha jioni wageni kutoka mataifa yanayoibukia katika sekta ya gesi asilia na mafuta duniani. Hafla hiyo fupi ilifanyika katika Hoteli ya Ramada Resort jijini, Dar es Salaam.

 

Wageni hao wako nchini kuhudhuria mkutano wa siku nne (4) wa kundi la nchi zinazoibukia katika sekta ya uzalishaji gesi asilia na mafuta ambao hufanyika kila mwaka. Jumla ya washiriki 50 kutoka mataifa hayo wanatarajia kushiriki mkutano huo, Tanzania ni moja wapo ya nchi zilizopo katika kundi hilo.

 

Akiwakaribisha katika hafla hiyo, Balozi Sefue alielezea kufurahishwa kwake na ushiriki wa nchi hizo katika mkutano huo na kuwatakia mafanikio katika mkutano huo.