Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI ASHIRIKI MKUTANO WA KUMI (10) WA WAKUU WA UTUMISHI WA UMMA WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA, PUTRAJAYA MALAYSIA 19-21 OKTOBA, 2014


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue, yuko mjini Putrajaya Malaysia kushiriki mkutano wa wakuu wa utumishi wa umma wa nchi wanachama wa jumuiya ya madola ulioanza tarehe 19 Oktoba, 2014.

Mkutano huu ambao unafanyika sanjari na maadhimisho ya miaka 10 ya Chama cha Wakuu wa Utumishi wa Umma wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola ulifunguliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia, Mhe. Muhyiddin Moh'd Yassin.

Wakati mkutano huu ukiendelea, mawaziri wanoshughulikia masuala ya Utumishi wa Umma kutoka katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola nao wamefanya mkutano wao wa tano (5) kuzungumzia masuala ya Utumishi wa Umma, katika mkutano huo Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mhe. Celina Kombani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Mada ya Mkutano wa mwaka huu ni "Mabadiliko katika Utumishi wa Umma; Mjadala Mapya" (Public Service Transformation: A New Conversation)