Habari
KATIBU MKUU KIONGOZI, ASHIRIKI KIKAO CHA 9 BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA(TNBC), IKULU, 2 OKTOBA, 2015
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue tarehe 2 Oktoba 2015 ameshiriki katika kikao cha tisa (9) cha Baraza la Taifa la Biashara kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu, DSM.
Kikao hicho kimeendeshwa chini ya Mwenyekiti wa Baraza, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisaidiana na Mwenyekiti Mwenza, Dkt. Reginald Mengi.
Kikao hicho kililenga, pamoja na mambo mengine, kupitia hatua za utekelezaji wa maazimio ya kikao cha 8 kilichofanyika tarehe 2 Septemba, 2015.
Akimkaribisha Mwenyekiti wa Kikao, Balozi Sefue alieleza kuwa vikao vya Baraza vinalenga kutafuta njia na suluhisho madhubuti za kuimarisha mazingira ya kibiashara kama vile kurahisisha upatikaji wa leseni, ardhi ,uhuishaji wa kodi , vibali vya makazi kwa wawekezaji, na kadhalika.
Aidha, Balozi alimpongeza Mheshimiwa Rais kwa uongozi madhubuti na kwa hatua kadhaa alizochukua wakati wa uongozi wake kuimarisha mahusiano kati ya serikali na wafanyabiashara. Na kwa niaba ya wajumbe wa Baraza alimtakia afya njema wakati wote.
NB: Hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi inapatikana katika tovuti hii