Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI ASHAURI SERIKALI ZA KIAFRIKA ZISISUBIRI MATOKEO YA TATIZO ILI KUCHUKUA HATUA ZA KUDHIBITI, CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA, KUNDUCHI DAR ES SALAAM, 28 MEI, 2015


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo tarehe 28 Mei, 2015 katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam, ametoa rai kuwa Serikali za Kiafrika zisisubiri matokeo ya tatizo ili kuchukua hatua za kudhibiti tatizo wakati limeshatokea (reactive) na badala yake zichukue hatua za kudhibiti tatizo kabla halijatokea (proactive).

 

Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa akiwasilisha mada kuhusu … Changamoto za Utumishi wa Umma katika Ngazi za Maamuzi ya Kisera kwa washiriki wa Mafunzo ya Uongozi katika chuo hicho kutoka nchi mbalimbali za Afrika na pia washiriki kutoka Taasisi za Serikali nchini.

 

.Dunia ya leo inahitaji Serikali kuwa makini, tayari na inayotangulia kuyashughulikia matatizo kabla hayajatokea. Akasisitiza kwamba ni vema serikali zikasimamia vizuri matarajio ya wananchi kila fursa za maendeleo zinapojitokeza.

 

NB: Mada ya Katibu Mkuu Kiongozi inapatikana kwenye tovuti hii.