Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

Katibu Mkuu Kiongozi akutana na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Japan na Balozi wa Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kwa Maendeleo ya Africa Bw. Junzo Fujita. 19 Agosti, 2016


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Mhandisi John W. H. Kijazi, leo tarehe 19 Agosti, 2016 amefanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Japan na Balozi wa Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kwa Maendeleo ya Africa Bw. Junzo Fujita, ambaye alimtembelea Katibu Mkuu Kiongozi ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Bw. Fujita ambaye aliambatana na Balozi wa Japan Nchini, Mhe. Masaharu Yoshida na Afisa Mwandamizi katika ubalozi huo, Bi. Tasnim Akbar, aliusifu uhusiano mzuri wa Nchi yake na Tanzania na aliwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi yake, Mhe. Shinzo Abe kwa serikali ya Tanzania.

Akitoa shukrani zake Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Mhandisi John W. H. Kijazi, aliishukuru sana serikali ya nchi ya Japan kwa kuwa mshirika na mdau mkubwa wa maendeleo ya Tanzania na kusisitiza kuwa ushirikiano huu utaimarishwa kwa manufaa ya pande zote mbili.