Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA BI. VALERIE MARCEL WA CHATHAM HOUSE, LONDON 12 MEI, 2015


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, amekutana na Bi. Valerie Marcel, Mchunguzi Mshiriki kutoka Chatham House, London. Bi. Marcel aliambatana na Bw. Rajkumar Singh wa Natural Resource Governance Institute (NRGI) - Tanzania na Bw. Dennis Rweyemamu kutoka Taasisi ya UONGOZI.

Mazungumzo yao yalihusu maandalizi ya Mkutano wa Kundi la Nchi Zinazoibuka katika Uzalishaji wa Mafuta (New Petroleum Producers Group) uliopangwa kufanyika hapa nchini tarehe 30 Juni - 1 Julai, 2015 kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania, Chatham House na Taasisi ya UONGOZI.