Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA BALOZI WA PALESTINA MHE. DKT. NASRI ABUJAISH LEO SEPTEMBA 26, 2014.


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue leo tarehe 26 Septemba, 2014 amekutana na Balozi wa Palestina nchini ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baada ya utambulisho, Dkt. Abujaish alipata fursa ya kuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi. Katika mazungumzo yao, suala la msingi lililojitokeza ni kuhusu kuendeleza uhusiano wa muda mrefu wa Kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili, yaani Tanzania na Palestina hususan uhusano wa Diplomasia ya Kiuchumi.

Masuala mengine yaliyojitokeza katika mazungumzo hayo yalihusu mgogoro wa mpaka kati ya Palestina na Isreli, na fursa zilizopo katika sekta za Utamaduni, Elimu na Utalii katika nchi hizi. Mazungumzo ya viongozi hao yalichukua takriban muda wa dakika ishirini (20).

Mwisho Balozi Dkt. Abujaish alishukuru kwa kupata nafasi ya kumtembelea Katibu Mkuu Kiongozi na kuwa na mazungumzo naye ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana naye tangu alipoteuliwa kuiwakilisha nchi yake nchini Tanzania.