Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA BALOZI WA FINLAND NCHINI.


Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue amekutana na Balozi wa nchi ya Finland nchini Tanzania Mhe. Sinikka Antilla ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 27, 2014.

 

Balozi Antilla ndiye Mwenyekiti wa Kundi la Nchi 12 Washirika wa Maendeleo zinazosaidia bajeti ya Tanzania (General Budget Support Group), na amechukua nafasi hiyo tangu mwezi April mwaka huu.

 

Lengo la Balozi Antilla  kuonana na Katibu Mkuu Kiongozi ni kujitambulisha kwa wadhifa huo mpya na kueleza jinsi atavyotekeleza jukumu hilo la Uenyekiti. Pamoja na hilo Balozi Antilla ameelezea vipaumbele walivyojiwekea katika kuchangia bajeti ya serikali na wakabadilishana mawazo ya namna ya kuimarisha mjadala (dialogue) kati ya kundi hilo la nchi washirika wa maendeleo na Tanzania.