Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

Katibu Mkuu Kiongozi ahudhuria Mkutano wa 11 wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa Nchi Wanachama wa a Jumuiya Ya Madola Kutoka Afrika (11th Forum for Commonwealth Heads of African Public Service) Mjini Port Louis, Mauritius, 8 Julai, 2014


Katibu Mkuu Kiongozi,  Balozi Ombeni Y. Sefue yupo mjini Port Louis Mauritius kuhudhuria Mkutano wa 11 wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kutoka Africa ulioanza leo tarehe 8 Julai 2014.

 Katibu Mkuu Kiongozi anaongoza ujumbe wa Tanzania unaowashirikisha Bwana George Yambesi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bwana Jumanne Sagini, Katibu Mkuu, Ofisi wa Wziri Mkuu (TAMISEMI), Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao. , Bwana Priscus Kiwango, Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Bwana Baraka Luvanda, Mratibu katika Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi.

Mada kuu ya Mkutano wa mwaka huu ni “Serikali Mtandao kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu”

Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Rais wa Mauritius, Mhe. Rajkeswur PURRYAG ambaye aliwakaribisha washiriki na kuwatakia mkutano wenye mafanikio. Rais PURRYAG alisisitiza kuwa matumizi ya TEHEMA katika uendeshaji wa nchi, taasisi za Umma na binafsi na pia katika  maisha ya kila mmoja hayakwepeki katika karne hii.

 “Matumizi ya TEHAMA yanawezesha kubadili namna jamii moja inavyohusiana(interrelate) na jamii nyingine” alisisitiza Rais PURRYAG. “

“Ni muhimu kuimarisha matumizi ya TEHAMA ili yaweze kutuletea maendeleo ya watu wetu,kupunguza umaskini wa watu wetu, kupunguza tatizo la ajira na ia kuboresha elimu na afya ya watu wetu,” alisema.

Mkutano huu ambao hufanyika kila mwaka utamalizika tarehe 10 Julai,2014 na unatarajiwa kuazimia ,pamoja na mambo mengine kuhusu umuhimu wa matumizi ya TEHAMA katika kuboresha utoaji huduma kwenye taasisi za umma na za binafsi kwa wananchi na kuongeza uwazi na uwajibikaji.