Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

Katibu Mkuu Kiongozi agawa Vitambulisho aya ziada vya Wajasiriamali wadogo wa Mkoa wa Dar Es Salaam.


Leo tarehe 15 Januari, 2019 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John W. H. Kijazi aligawa Vitambulisho 75,000 kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abubakar M. Kunenge. Huu ni muendelezo wa uzinduzi wa Vitambulisho hivyo uliofanywa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akifungua Mkutano wa Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa uliofanyika tarehe 10 Desemba, 2018 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere – Dar es Salaam. Wakati wa uzinduzi huo, kila Mkuu wa Mkoa alipewa Vitabulisho Ishirini na tano elfu (25,000) kwa ajili ya kugawa kwa Wajasiriamali Wadogo.

Hafla ya ugawaji wa vitambulisho hivyo ilihudhuriwa na Bw. Andrew Massawe, Katibu Mkuu, Ofisi wa Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira Vijana na Wenye Ulemavu; Mhandisi Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu TAMISEMI na Bw. Charles Kichere, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.