Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI AFUNGUA KONGAMANO MAALUM (LABORATORY WORKSHOP) LA KUPITIA PROGRAMU YA MAGEUZI YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU CHINI YA MAABARA YA TEKELEZA KWA MATOKEO MAKUBWA SASA! (BRN), LILILOFANYIKA KATIKA HOTELI YA KUNDUCHI 16 MACHI, 2015.


Katibu Mkuu Kingozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo tarehe 16 Machi, 2015 amefungua Kongamano maalum lililoandaliwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kupitia Mfumo Mahsusi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu nchini chini ya utaratibu wa maabara (Lab approach) wa BRN. Kongamano hilo linafanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo litakalofanyika kwa muda wa wiki tatu (3) limelenga pamoja na mambo mengine kuweka mifumo wezeshi ya Ubunifu hapa nchini itakayohusisha sekta zote na jamii yote ya Kitanzania kufikia malengo yaliyo kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 inayolenga kujengwa kwa jamii yenye maarifa (Knowledge - based society).

Akielezea umuhimu wa Sanyansi, Teknolojia na Ubunifu, Katibu Mkuu Kiongozi alisisitiza kuwa vitu hivyo vitatu, ndivyo vimesaidia nchi zote zilizoendelea kufikia hatua hiyo ya maendeleo, kwa hiyo si jambo la hiari bali la lazima kwa maendeleo ya nchi yetu.

NB: Soma hotuba nzima ya ufunguzi ya Katibu Mkuu Kiongozi, kupitia tovuti hii