Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

KATIBU MKUU KIONGOZI AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAAZI WA BENKI YA DUNIA NCHINI, BW. PHILLIPE DONGIER, DODOMA, 20 MACHI, 2015


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, leo tarehe 20 Machi, 2015 amekuwa na mazungumzo na Mwakilishi Mkaazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Phllipe Dongier kuhusu ushirikiano wa Tanzania na benki hiyo.

Mazungumzo ambayo yalifanyika katika Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyopo katika jengo la TAMISEMI, Mjini Dodoma yalihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile, Kamishana wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Bw. Ngosha Said Magonya na Maafisa wengine kutoka Wizara ya Fedha na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri.

Mazungumzo hayo yalijikita zaidi katika misaada ambayo benki ya dunia inaipatia Tanzania ambayo ni pamoja na Misaada ya Kibajeti (Budget Support), Miradi ya Kilimo katika Ukanda wa Kusini (SAGCOT PROJECTS) na kuhusu Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART).

Katibu Mkuu Kiongozi yupo kikazi mjini Dodoma tangu tarehe 16 Machi, 2015.