Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

Katibu Mkuu Kiongozi atembelea Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane mjini Mbeya – 7 Agosti, 2023


Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe.Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka leo tarehe 7 Agosti 2023  ametembelea mabanda mbalimbali ya Wizara, Wakala, Taasisi na Wadau wa sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane katika Viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.

Akiwa kwenye Viwanja hivyo, Balozi Kusiluka amepata taarifa mbalimbali za bidhaa na huduma zinazotolewa na Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Taasisi, Wakala na Bodi zilizo chini ya Wizara hizo.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja watendaji kutoka ofisini kwake.