Habari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemteua Balozi John W. H. Kijazi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA).

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemteua Balozi
John W. H. Kijazi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za
Serikali (TGFA).
Uteuzi
wa Mhe. Balozi Kijazi ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi umeanza tarehe 26
Februari, 2020
Ifuatayo
ni orodha ya wajumbe wa Bodi hiyo:-
1.
Dkt.
Leonard M. CHAMURIHO - Katibu Mkuu (Uchukuzi), Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
2.
Balozi
Kanali Wilbert IBUGE - Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
3.
Mhandisi
Ladislaus MATINDI – Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Ndege, Tanzania (ATCL).
4.
Mhandisi
Julius NDYAMUKAMA – Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege, Tanzania (TAA).
5.
Valite
G. MWASHUSA – Kikosi cha Ulinzi wa Viongozi.
6. Kapt. Narzis A. KISIMBO – Rubani, Wakala wa Ndege za Serikali.........