Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Habari

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue akutana na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Mt. Thomas cha Minnesota, Marekani, tarehe 16 Julai, 2014


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue leo tarehe 16 Julai, 2014 amekutana na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt. Thomas cha Minnesota, Marekani wanaotembelea Tanzaniakujifunza uzoefu wa Tanzaniakatika masuala ya kiuongozi na anuwai za tamaduni. Wanafunzi hao ambao kwa idadi yaoni wanafunzi 14 wanaochukua Shahada za Uzamili na Uzamivu katika masuala ya uongozi wa kimataifa pamoja na Wakufunzi wao wawili, Dr. Jean-Pierre Bongila na Dr. Artika Tyner.

 

Mkutano huu ni mwendelezo wa mkutano kama huu ambao Katibu Mkuu Kiongozi aliufanya mwaka jana na kundi jingine la wanafunzi kutoka Chuo hicho ambapo aliwapa uzoefu wa uongozi na anuwai ya tamaduni katika   Tanzania, Afrika na katika medani za kimataifa.

 

Kwa kutambua umuhimu wa nasaha walizozipata wanafunzi wa mwaka jana, Chuo hicho kiliomba na kukubaliwa fursa nyingine ya kuonana na Katibu Mkuu Kiongozi.

 

Ziara ya wanafunzi hao ilianzia Arusha tangu tarehe 12 Julai, 2014 na itamalizika tarehe 17 Julai,2014.

 

Pamoja na kupata fursa ya kuonana na kuzungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Arusha, wanafunzi hao walipata pia muda wa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Arusha na baadayezanzibar. Na matarajio ni kuwa wanafunzi hao watakuwa mabalozi wazuri wa kuitangazaTanzaniasehemu mbalimbali za dunia watakakokwenda kufanya kazi.