Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Wasifu

Balozi Marten Y.C. Lumbanga
Balozi Marten Y.C. Lumbanga
Balozi

Elimu

Balozi Lumbanga alitunukiwa Shahada ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam machi 1972. Alipata Shahada yake ya Uzamili katika masuala ya Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo cha Diplomasia na Mahusiano ya Kimataifa cha Geneva  (Geneva School of Diplomacy and International Relations). 

Historia Kwa Ufupi

Balozi Dkt. Martin Y.C. Lumbanga aliapishwa kuwa Katibu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma mwaka 1996. Aliwahi pia kuitumikia Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania katika nyadhifa mbalimbali. Kuanzia mwaka 1986 alipoteuliwa kushika nyadhifa za Ukatibu Mkuu katika Wizara mbalimbali mpaka alipoteuliwa kushika wadhifa huo wa juu katika utumishi wa umma na Baraza la Mawaziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nafasi aliyoitumikia kwa kipindi cha miaka kumi namoja kuanzia Februari 1995 hadi Januari 2006. Katika kipindi hiki alihusika na mabadiliko mbalimbali katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ndani ya utumishi wa umma. Kuanzia mwezi February 2006, Balozi Lumbanga aliteuliwa kuwa Balozi na Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Kudumu za Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa Geneva, Uswizi. Na pia aliwakilisha katika ofisi za Umoja huo za Vienna, Austria. Toka aliporudi nyumbani Tanzania, Balozi Lumbanga aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (Public Procurement Regulatory Authority (PPPA) ) na Mhe. Jakaya M. Kikwete, Rais wa Awamu ya nne.