Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Wasifu

Balozi Ombeni Yohana Sefue
Balozi Ombeni Yohana Sefue
Balozi

Elimu

Balozi Sefue amesomea masuala ya Utawala wa Umma katika Taasisi ya Usimamizi wa Maendeleo - Mzumbe (sasa Chuo Kikuu Mzumbe) na kutunukiwa Stashahada ya Daraja la Juu katika Masuala ya Utawala wa Umma mwaka 1977.

Mwaka 1981 alipata Shahada ya Uzamili katika masuala ya Sera na Utawala kutoka Institute of Social Studies (ISS), (sasa inajulukana kama The International Institute of Social Studies of Erasmus University), mjini The Hague, Uholanzi

Mwaka 1986 alipata mafunzo katika ngazi ya cheti katika masuala ya Mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia kutoka Kituo cha Mafunzo ya Diplomasia cha Tanzania na Msumbiji (Sasa Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam)

Pia amepata mafunzo ya Upatanishi wa Kimataifa kutoka  International Peace Academy, na  mafunzo kuhusiana na changamoto za kuchumi na kijamii katika nchi zinazoendela kutoka  International Relations and Socialist Integration with the Presidium of the Bulgarian Academy of Sciences (1984).

 

Balozi Ombeni Yohana Sefue aliapishwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 31 Disemba, 2011. Kama Katibu Mkuu Kiongozi, yeye ni Katibu wa Baraza la Mawaziri na Mkuu wa Utumishi wa Umma.

Nafasi za Kiutendaji

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa mjini New York tangu Agosti 31, 2010.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mwakilishi Nchini Mexico, Juni 2007 hadi Agosti, 2010

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada na Mwakilishi Nchini Cuba, Oktoba 2005 hadi Juni, 2007

Balozi Sefue alikuwa Mwanadiplomasia na Mshauri katika Ubalozi wa Tanzania mjini Stockholm, Sweden 1987 hadi 1992

Kati ya mwaka 1993 na 2005, alifanya kazi ya uandishi wa hotuba  na Msaidizi kwa Marais wawili wa Tanzania, Rais Ali Hassan Mwinyi (1993-1995) na Rais Benjamin W. Mkapa (1995-2005)