-


Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu namna ya kuadhimisha siku ya Uhuru yaani Tarehe 9 Desemba, 2015 kuwa siku hiyo sio siku ya mapumziko.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni  Sefue, amesema siku hiyo ni siku ya kazi kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Mamlaka aliyonayo kisheria.

Katika ufafanuzi huo, Balozi Sefue amesema endapo wafanyakazi watakuwa na kazi muhimu za kufanya katika ofisi zao wanaweza kwenda kazini kama kawaida, vinginevyo washiriki kufanya usafi katika maeneo wanayoishi au maeneo yanayozunguka sehemu zao za kazi.

Aidha, amesisitiza kuwa kampeni ya usafi itafanywa nchi nzima na kuwasihi viongozi katika mamlaka za serikali za mitaa kulisimamia zoezi hilo kwa ukamilifu.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

08 Desemba, 2015.