Katibu Mkuu Kiongozi apokea taarifa ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa “Standard Gauge” kutoka Dar es salaam hadi Morogoro – 19/07/2017


Jul 20, 2017

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mha., John W. H. Kijazi leo tarehe 19/07/2017 amepokea taarifa ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa “Standard Gauge” kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkezi ya kutoka nchini Uturuki Bw. Erdem Ariouglu.

Kampuni ya Yapi Merkezi ilishinda kandarasi ya ujenzi huo na mnamo Aprili 12, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliuzindua mradi huo kwa kuweka jiwe la msingi katika eneo la Pugu stesheni, Jijini Dar es salaam.

Katika uwasilishaji wa ripoti hiyo Bw. Ariouglu aliambatana na Mhandisi Kemal Fuat Uzun, ambaye ni Meneja Mradi anayesimamia masuala ya utawala.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi, aliahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri ili kuhakikishamradi huo unakamilika katika muda uliopangwa.