Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemteua Balozi John W. H. Kijazi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA).

Feb 29, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemteua Balozi John W. H. Kijazi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA).

Uteuzi wa Mhe. Balozi Kijazi ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi umeanza tarehe 26 Februari, 2020

Ifuatayo ni orodha ya wajumbe wa Bodi hiyo:-

1. Dkt. Leonard M. CHAMURIHO - Katibu Mkuu (Uchukuzi), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

2. Balozi Kanali Wilbert IBUGE - Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

3. Mhandisi Ladislaus MATINDI – Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege, Tanzania (ATCL).

4. Mhandisi Julius NDYAMUKAMA – Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Tanzania (TAA).

5. Valite G. MWASHUSA – Kikosi cha Ulinzi wa Viongozi.

6. Kapt. Narzis A. KISIMBO – Rubani, Wakala wa Ndege za Serikali........